
Wanachama wa CCM shina la Hunan- Changsha waliweza kukutana na kufanya kikao cha pamoja kwa mujibu wa katiba ya CCM, SEHEMU YA TATU, ibara ya 24 na 25. Kama shina tulitembelewa na Comrade Manini Daudi Romani ambaye ni mwenyekiti wa Tawi la CCM China na mgeni rasmi wa mkutano wetu.
Comrade Manini aliweza kuwagawia kadi baadhi ya wanachama waliokuwa wameiva kiitikadi na kutimiza vigezo.
Pia comrade Manini amewaasa na kusisitiza kwa wanachama mambo makuu matatu kama ifuatavyo:
- Kuendelea kutangaza na kusema mambo mema na makubwa yanayofanywa na serikali ya chama cha mapinduzi chini ya Dr Samia Suluhu Hassan na Dr Hussein Ali Mwinyi katika kuwaletea maendeleo watanzania.
- Kuwaasa watanzania kuendelea kukiamini na kukiunga mkono chama cha mapinduzi, kukipigia kura za kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa na ule wa urais, ubunge na udiwani.
- Kutumia fursa za kimasomo zinazo patikana nchini China kwa lengo la kujielimisha na kutumia maarifa hayo kwa maslahi mapana ya Taifa.
Vilevile Mwenyekiti wa shina Ndg Bernard H. Manyama alimshukuru mgeni rasmi na wanachama wote kwa kutenga muda wao na kujumuika kwenye mkutano na kusisitizaa kuendelea kuwa wazalendo katika kuisemea mema nchi yetu na chama kwa ujumla.
Uongozi wa Shina unatoa pongezi kwa wajumbe wote na wanachama walioweza kuhudhuria katika mkutano hicho.
