Faruku Maulid Mpare

MWENYEKITI (2024-To Date)

Anafanya shada ya Uzamivu katika chuo kikuu cha kaskazini mashariki mwa China (Northeast Normal University )

Juliana Gaithan Kauno

KATIBU (2024-To Date)

Anafanya shada ya Uzamivu katika chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha China (University of Science and technology of china USTC)

Chama Cha Mapinduzi (CCM) shina la Jilin-China ni miongoni mwa mashina makongwe ya CCM nchini China. Shina hili lilikua hai na imara sana mpaka mwaka 2019 wakati ulipoibuka ugonjwa hatari wa Homa ya Mapafu (UVIKO) nchini China. Ugonjwa huo ulipelekea waliokuwa wanachama wa CCM, shina la Jilin kurejea haraka nyumbani Tanzania na kuacha shina likiwa halina wanachama. Hali hiyo ilidumu mpaka mwishoni mwa mwaka 2022 ambapo China ilifungua tena mipaka yake na kupelekea wanafunzi na watanzania wengine kuruhusiwa kurejea China. Mpaka kufikia mwaka 2023 tuliweza kupata jumla ya wanachama wapya 23. Pia mwaka huu shina limefanikiwa kuchagua viongozi wake, Mwenyekiti wa chama ni Faruku Maulid Mpare na katibu ni Juliana Gaithan Kauno.

 

Address: No. 5225 Renmin Street, Chaoyang District, Changchun
Phone: 15143085140