
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akiongozana na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi akiwemo Katibu wa NEC – Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Cde. Rabia Abdalla Hamid walipata kulitembelea Tawi la CCM China likiwakilishwa na wanachama kutoka mashina mbalimbali likiwemo shina la Beijing, mjini Beijing, nchini China katika hoteli ya Wanshou, tarehe 28/08/2024, siku ya J.tano.
Tawi la CCM China linapenda kutoa shukrani za dhati kwa Viongozi wetu hao kwa kulitembelea Tawi letu, kwa hakika tumejifunza mengi, kwa pamoja tunasema ASANTENI SANA NA KARIBUNI TENA!
TUNAZIMA ZOTE, TUNAWASHA KIJANI!
