
Katibu wa CCM Tawi la China Cde Amedeus Komu amekutana na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Mh Rabia A. Hamid kwenye Ofisi ndogo za CCM zilipo Lumumba Dar-es-salaam. Katika kikao hiko Cde Rabia amelipongeza Tawi la China kwa kazi nzuri wanazizofanya na kusisitiza kuendelea kukisemea vizuri Chama na Serikali yake kwa mambo makubwa yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dr Hussein Ali Mwinyi.
Cde Rabia ametumia nafasi hiyo kulipongeza Tawi la CCM-China kwa msaada wa madaftari zaidi ya 2400 na kalamu zaidi ya 1250 walioutoa kwa waathirika wa Mafuriko ya Hanang yaliyotokea mwishoni mwa mwaka 2023.
Naye Cde Komu akitoa salamu za Tawi la China kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tawi la CCM-China Cde Daudi R Manin amemshukuru sanaa Katibu wa NEC-SUKI kwa kuwa karibu na Tawi la CCM China. Na kuahidi kuwa CCM-China itaendelea kuunga mkono kazi kubwa zinafonywa na Serikali ya CCM. Pia amemuomba kufikisha salamu nyingi za pongezi kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza mahusiano mazuri ya Tanzania na China ambayo yamefungua fursa za ufadhili wa masomo kwa watanzania zaidi ya 1000 kila mwaka wanapata nafasi ya kwenda nchini China kwa masomo na zaidi ya wafanyabiashara 500 kila mwezi wanaenda China kibiashara.
