
Shina la Hunan limefanya makabidhiano ya kiungozi baada ya viongozi waliyo pita kumaliza muda wao wa mwaka mmoja wa kulitumikia shina, viongozi waliyomaliza muda wao ni Mwenyekiti Ndg. BERNARD HAMENYA MANYAMA, Katibu Ndg. MUHAMED AMOUR FOUM na Mwenezi Bi. AWENA ABDISALAM ALI. Mwenyekiti anayemaliza muda wake aliweza kumkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti mteule Ndg. HUSSEIN ALLY KANDURU. Sambamba na hilo vilevile Mwenyekiti wa tawi la CCM China Dr. MANINI DAUDI ROMANI aliweza kuwagawia vyeti vya pongezi kwa viongozi wote waliyomaliza muda wao na wanachama waliyo hitimu kwa ujumla.
