
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dr.Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 06/09/2024 alikutana na Watanzania waliopo China mongoni mwao ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi tawi la China katika Ukumbi wa BVLGARI Beijing Hotel.
Mhe. Rais alizungumzia mafanikio ya Tanzania ambayo kwa sasa yanatekelezwa ndani ya 4Rs (Maridhiano, kustahmiliana, Kufanya mageuzi, na kujenga upya Taifa letu) alisema: ukuaji wa uchumi mwaka 2024 ni asilimia 5.3 na unategemea kufikia asilimia 6 hadi 6.5 mwaka 2025. Suala la mfumuko wa bei limeendelea kuwa stable kwa asilimia 3 kwa takribani miaka 5 sasa (2019~2024). Kukamilika kwa bwawa la Mwl Nyerere ambalo ni kati ya miradi ya kimkakati, kuendela na mradi ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) Rwanda na Burundi. Haya ni Mapinduzi makubwa ya kiuchumi.
Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari, Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 147 mwaka 2023 hadi 97 mwaka 2024 duniani. Mhe. Rais alisema serikali itaendeleza utalii na kuvutia wawekezaji kwani ni sector muhimu kwa uchumi wa Tanzania.
Pamoja na mafanikio hayo, Mhe. Rais aliongelea changomoto zilizowasilishwa na makundi tofauti yaliyoshiriki ambayo ni wanafunzi, wafanyakazi, wafanyabiashara na waakazi. Akizungumzia suala la Bima Ya Afya, Mhe Rais alisema Serikali itaangalia utaratibu mzuri kwa wenye Bima ambao hautaingilia sheria na utaratibu wa Serikali ya China, suala la baadhi ya vyuo vya China kutotambulika na TCU ameshauri waombaji wa scholarship kuzingatia viwango (standards) zinazotolewa na TCU, na suala la gharama za usafirishaji wa mizigo pamoja na maiti amelipokea.
Aidha, Mhe. Rais ameahidi kuongeza ndege nyingine kwa ajili ya safari za China. Pamoja na hilo Mhe. Rais amewasistiza watanzania wanapofika China wajisajiri kwenye JUMUIYA zao kwani hili litasaidia kupata taarifa zao kupitia ubalozi wetu uliopo hata China. Mhe. Rais ameendelea kuhimiza umoja, mshikamano na kuwa mabalozi wazuri wa NCHI yetu.
Katika Ziara yake Mhe. Rais alitoa hotuba kwa marais wote wa Afrika mashariki, hii ni heshima kubwa sana aliyopewa na heshima kwa Taifa letu la Tanzania. Aidha, Serikali imesaini mkataba wa kuboresha reli ya TAZARA.
